UMEFUNGUA ukurasa sahihi kabisa wa kukupatia elimu juu ya uhusiano na mapenzi. Karibu mpenzi msomaji wangu katika All About Love ambayo kila siku inaibuka na mada nzuri zinazolinda uhai wa uhusiano na wenzi wetu.
Marafiki leo nitazungumzia juu ya jambo muhimu sana ambalo limekomaa kwenye jamii yetu. Ni jambo linaloweza kusababisha matokeo mabaya kwenye uhusiano lakini kwa bahati mbaya wengi hawalioni.
Wengi (hasa wanawake) wamejikuta wakiingia kwenye mtego unaosababishwa na kuondoa thamani ya mwenzi wako na kuihamishia kwa wengine na mwishowe usaliti hutokea.
Wengi (hasa wanawake) wamejikuta wakiingia kwenye mtego unaosababishwa na kuondoa thamani ya mwenzi wako na kuihamishia kwa wengine na mwishowe usaliti hutokea.
Chanzo cha yote hayo ni mazoea mabaya ya kuitana majina ya kimapenzi na wanaume wengine, ambao si wenzi wake.
Hujawahi kumsikia mwanamke anamwita mwanaume ambaye si mpenzi wake kwa majina ya kimapenzi kama baby, sweetie, honey, mpenzi na mengine yanayofanana na hayo?
Majina ya kimapenzi yana thamani kubwa sana na ni vyema basi kama yakitumika kwa watu sahihi- wenzi husika.
Majina ya kimapenzi yana thamani kubwa sana na ni vyema basi kama yakitumika kwa watu sahihi- wenzi husika.
Ni maneno yenye mshawasha mkubwa na huonesha penzi la dhati lililopo moyoni mwa mhusika kwenda kwa mpenzi wake.
Husisimua na kuongeza ladha ya mapenzi ya kweli. Kumuita mpenzi wako kwa majina ya kimapenzi huongeza zaidi upendo na msisimko wa moyo.
Mwenzi hujiona wa kipekee na mapenzi huzidi kukua.
Kwa maana hiyo basi, ni sahihi zaidi kwa wapenzi kuitana majina niliyotaja hapo juu na mengine yanayofanana na hayo kwa lugha yoyote ile inayotambulika na anayeitwa.
Kwa maana hiyo basi, ni sahihi zaidi kwa wapenzi kuitana majina niliyotaja hapo juu na mengine yanayofanana na hayo kwa lugha yoyote ile inayotambulika na anayeitwa.
TUANGALIE ATHARI ZAKE
Majina niliyotaja hapo juu husisimua na kuongeza mapenzi. Kwa kuyatumia vinginevyo, basi kwa kiasi kikubwa huanza kukuathiri na kupunguza thamani ya neno lenyewe.
Kama unaweza kumuita mfanyakazi mwenzako dear, mtu wa jinsi sawa na wewe sweet ni wazi hata utakapomuita mpenzi wako au wewe kuitwa na yeye, halitakuwa na nguvu sana ya mapenzi kwa sababu ni neno ulilolizoea kila wakati.

HARUFU YA USALITI
Wakati mwingine unaweza kujikuta umeingia kwenye usaliti bila kutarajia. Juliana, mkazi wa Mikocheni jijini Dar es Salaam, alitoa ushuhuda ufuatao:
Wakati mwingine unaweza kujikuta umeingia kwenye usaliti bila kutarajia. Juliana, mkazi wa Mikocheni jijini Dar es Salaam, alitoa ushuhuda ufuatao:
“Mimi naishi na mchumba wangu, tuna mtoto mmoja mwenye miaka mitatu. Nafanya kazi saluni moja ya kiume. Tangu nimeanza hii kazi, nimejifunza kutumia maneno matamu ya kuwafurahisha wateja na wakati mwingine kuwafanya wanipe tipu baada ya kumaliza kazi.
“Kuna kaka mmoja nilizoeana naye sana. Kama kawaida, huwa namkaribisha kwa kumuita dear au sweet. Wakati nikiendelea kumfanyia scrub, mazungumzo yetu hutawaliwa na dear, sweet, nikajikuta nimezidi kumzoea.
“Kwa sababu tulibadilishana namba, mara akaanza kuwa na mazoea ya kunitumia meseji, akija ananipa pesa, anaondoka. Mazoea yakazidi. Nikajikuta nimemzoea na kuna siku ambayo siwezi kuisahau kabisa.
“Ni siku niliyomsaliti mchumba wangu...mbaya zaidi na huyo jamaa naye ana mke wake. Niliumia sana, lakini naamini kama nisingekuwa na mazoea ya kumuita majina ya kimapenzi nadhani nisingeingia mtegoni. Moyo wangu unauma sana, najuta kumsaliti mpenzi wangu.”
Unaweza usione athari hii moja kwa moja, lakini ndugu yangu chukua jambo hili leo; wanaume wengi wakiitwa kwa majina ya kimapenzi husisimka na hujiona wenye bahati na mara hushawishika kuingia mapenzini.
Kama mwanamke hatakuwa makini atajikuta ametumbukia. Ya nini yote hayo, wakati unaweza kubadilisha mazoea hayo?
MWISHO KABISA
Kati ya majina niliyoyataja, kuna ambayo yanakubalika kutumiwa na wasio na uhusiano wa kimapenzi lakini ni undugu wa damu. Mathalani baba, mama, kaka, dada, shangazi nk.
Kati ya majina niliyoyataja, kuna ambayo yanakubalika kutumiwa na wasio na uhusiano wa kimapenzi lakini ni undugu wa damu. Mathalani baba, mama, kaka, dada, shangazi nk.
Hakuna tatizo kumuita mtu mpendwa, lakini siyo baby, sweet, mpenzi na mengine yenye maana ya moja kwa moja ya kimapenzi.
Bila shaka somo limeeleweka na utachukua hatua.
Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Saikolojia ya Uhusiano anayeandikia Magazeti ya Global Publishers. Kwa sasa anaandaa kitabu chake kipya cha Maisha ya Ndoa.
Bila shaka somo limeeleweka na utachukua hatua.
Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Saikolojia ya Uhusiano anayeandikia Magazeti ya Global Publishers. Kwa sasa anaandaa kitabu chake kipya cha Maisha ya Ndoa.
0 comments:
Chapisha Maoni