10:00
0

Thea na Mike katika pozi.
WASANII wawili nyota wa filamu Bongo, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ na Michael Sangu ambao awali walitengana kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi, hatimaye wamerudiana.
Kikizungumza na gazeti hili, chanzo makini kutoka ndani ya familia hiyo kilisema wanandoa hao wamerudiana baada ya kupatanishwa na viongozi wa dini na familia zao, wakitelekeza viapo vyao vya awali kuwa kamwe wasingeishi tena pamoja.
“Thea na Mike wamerudiana, yaani waliitwa na padri na kuzungumza nao kwa kina na kuwauliza matatizo yao yalipoanzia hadi wakafikia kuachana, kila mmoja alitoa dukuduka lake huku na wanafamilia wakikaa na kuzungumza nao kwa kina na muafaka ulifikiwa na sasa wanaishi pamoja,” kilisema chanzo hicho.
Nyota wa filamu Bongo, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Mike na kumuuliza kuhusu suala hilo, ambapo alikiri na kusema anamshukuru Mungu kwani ndiye aliyewaunganisha tena.
“Namshukuru Mungu kwani ndiye muweza, kila mmoja aliyatambua makosa yake kwa hiyo tumeanza maisha mapya tofauti na zamani,”alisema Mike.
Staa katika filamu za Kibongo, Michael Sangu.
Kwa upande wake, Thea alipoulizwa alichekacheka na kumtaka mwandishi wetu kusubiri, ingawa pia alisema anawashukuru kwa dua zao.
“Mh na nyie ni wambeya sana, mmeyajuaje hayo! naomba msiwe na haraka na ninashukuru sana kwa dua zenu,”alisema Thea.
- See more at: http://mdadisihuru.blogspot.com/2014/05/thea-na-mike-warudiana-kimapenzi.html#sthash.KWIoRtiH.dpuf

0 comments:

Chapisha Maoni

rightcolbanner