04:15
0

Nina wasiwasi na uwakilishi wa baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, ninajiuliza je, wataweza kutimiza jukumu walilopewa na Watanzania na Rais Jakaya Kikwete la kusimamia mchakato wa kupata Katiba Mpya au la?

Wasiwasi wangu unasababishwa na jambo moja, kauli za baadhi ya wajumbe hasa ile ya kuanza kufikiria masilahi yao na kusimama kidete kutaka yatekelezwe bila kujali endapo yana athari kwa taifa. Wakiwa katika siku yao ya tatu, baadhi ya wajumbe walianza kuwatia kichefuchefu Watanzania kwa kulalamikia kiwango cha posho ya Sh300,000 na kutaka kiongezwe ili walau kifikie Sh500,000.

Ikumbukwe kuwa kila mjumbe wa bunge hilo anapokea Sh300,000 kama posho kwa siku awapo katika kikao cha bunge hilo.

Jambo baya zaidi ni kuwa wakati baadhi ya wajumbe wa bunge hilo wakidai nyongeza ya posho, tayari Watanzania walishaanza kuhoji iweje wapewe kiasi kikubwa hicho cha pesa

0 comments:

Chapisha Maoni

rightcolbanner