Ni uvurundaji wa maadili au shetani anawapitia?
Mila, utamaduni, desturi na ulinzi pia, vinaweza kuwa chanzo kikubwa kuingiza aibu kwenye majumba ya wakuu wa nchi zilizo Kusini mwa Afrika, Afrika Kusini (kwa Jacob Zuma) na Swaziland (kwa Mfalme Mswati III).
Na mwandishi wetu
Hivi karibuni, viongozi hao wa nchini zinazopakana wamejikuta wakikumbwa na skendo pacha za kusalitiwa na wake zao ambao ni miongoni mwa idadi kubwa ya wake waliowaoa ‘kihalali’.
Ukiweka pembeni habari ya mke wa 12 wa mfalme Mswati, Nothando Dube, 22 kukutwa ‘wakibanjuka’ hotelini na Waziri wa Sheria wa Serikali ya mumewe, Ndumiso Mamba, haijakatika miezi mingi, Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma naye alidaiwa kusalitiwa na mkewe, Nompumelelo Ntuli (Nantuli) aliyefunga naye ndoa mwaka 2008.
Habari za usaliti wa Nampumelelo ambaye alidaiwa kuzini na mlinzi wake, ziliibuliwa kwa mara ya kwanza mwaka jana na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo.
Hata hivyo, mume mtu Zuma alisema skendo ile ilipikwa kwa lengo la kumchafua jina ingawa hakuweka wazi, kwanini ‘mgoni’ wake huyo aliamua kujiua.
Ukiachilia mbali usaliti wa mke wa Zuma, Mfalme Mswati ambaye mpaka mwaka huu, 2010 unapiga hodi alikuwa na wake 13, habari zimesema huu kwake ni usaliti wa tatu.
Maumivu ya kwanza ya usaliti kwa Mfalme huyo ilikuwa mwaka 2004, wake zake wawili, Delisa Magwaza na Putsoana Hwala walitoa nje ya ndoa.
Tuachane na hao ambao pengine ‘ujana’ umechangia kujikuta wakikengeuka kwenye ndoa zao mara baada ya ‘hazbandi’ wao kuwa ‘bize’ na harakati za uongozi, lakini nachelea kuwa, huenda kuna upindaji wa maadili kwa wanawake walio Kusini mwa Afrika.
Kwa maana gani?
Wakati Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela ‘Madiba’ anatoka Gereza la victor-vorster kwenye kisiwa cha Robinson mwaka 1990, muda mfupi baadaye alimtaliki mkewe, Winnie Melekizedeki Mandela kwa madai ya kumtuhumu kutoka nje ya ndoa wakati ‘Mzee’ huyo akiwa kifungoni.
Inadaiwa kuwa, Winnie alikuwa ‘akichiti’ na kijana mmoja mjini Soweto, Sauzi na ‘hakuna mtu aliyekuwa hajui’.
Swali hapa linabaki kuwa, ni kwanini wake wa viongozi hao wamekuwa wakikumbwa na tuhuma nzito kama hizi? Je, kuna ukengeufu wa maadili Kusini mwa Afrika au ni shetani anawapitia?
Kwa mujibu wa jarida moja nchini Afrika Kusini, inaonekana mila na desturi pia inatoa mchango mkubwa katika kutokea kwa usaliti huu. Kitendo cha Mfalme Mswati kuwa na wake zaidi ya wawili (kumi na tatu) kinaweza kuchangia kwani mzunguko wa kindoa unaweza kuwa hafifu, hasa ikizingatiwa kuwa, nao ni binadamu.
Aidha, ulinzi huenda ukawa na mzigo wake wa lawama, kwani si rahisi kwa mke wa Kiongozi Mkuu wa nchi akapatikana hotelini bila Itifaki kujua amefuata nini kama ilivyotokea kwa Nothando Dube na Waziri wa Sheria wa Swaziland, Ndumiso Mamba.
Kama baadhi ya nchi zinavyopiga vita mila na desturi za kukeketa (kwamba zimepitwa na wakati) basi Swaziland na Afrika Kusini wanatakiwa kuamka na kupiga vita ‘utamaduni’ wa kiongozi wa nchi kuoa wake mpaka 13 la sivyo skendo za usaliti zitaendelea kuzitesa nchi hizo.
0 comments:
Chapisha Maoni