Uchafu! Picha za madiva wakubwa wa filamu Tanzania, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson zimebambwa na gazeti hili hivi karibuni wakiwa katika hali ya kimalavidavi licha ya kwamba, mmoja ni mke wa mtu, mwingine mchumba.
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu, ishu hiyo ilichukua nafasi maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam ambako Wema na Aunt wamepiga kambi kwa ajili ya filamu yao mpya ya Familia.
Ilidaiwa kuwa, Wema na Aunt ambao kwa sasa wapo ‘kloz’ kiasi cha watu kuwa na maswali vipi kuhusu Kajala Masanja, walipiga picha hizo wakidhamiria kuzifuta baada ya kujiona lakini lililotokea si akili zao, picha hizo zikanaswa na paparazi wetu.
Habari za ndani zinasema, baadhi ya ndugu wa mume wa Aunt, Sunday Dimonte wamekuwa wakimtumia meseji ‘mista’ huyo kumweleza uchafu mbalimbali anaofanya mume wake licha ya kutotoa tamko lolote.
0 comments:
Chapisha Maoni