MATUKIO ya uvunjifu wa maadili kwenye shule mbalimbali hapa nchini yameendelea kushamiri baada ya wanafunzi wanne wa Shule ya Msingi Lulanzi wilayani Kibaha mkoani Pwani kutuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili na kumsababishia maumivu yaliyopelekea kulazwa Hospitali ya Tumbi kwa matibabu.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana babu wa mtoto huyo, Jacob Mrope alisema tukio hilo lilitokea March 27 saa 6 mchana ambapo mjukuu wake ambaye ni yatima alikuwa akitoka shuleni huku akiwa na wenzake wawili wakike, walikimbizwa na watuhumiwa hao ambapo yeye alishindwa kukimbia kutokana na kuumia mguu na kujikuta akibakwa.
Mrope alisema kuwa wanafunzi wenzake aliokuwa nao walisema kuwa baada ya watuhumiwa hao kumkamata walimziba mdomo kisha wakaanza kumuingilia kwa zamu ambapo mwanafunzi huyo hakuweza kupata msaada wowote hadi watuhumiwa hao kutimiza haja zao.
"Wenzake waliokuwa nao walitoa taarifa nyumbani kwa mlezi wake ambaye ni dada yake ambapo alikwenda na kumkuta akitokwa na damu nyingi na alipomuuliza alisema kuwa wenzake wamembaka ndipo alimchukua na kumpeleka shuleni kutoa taarifa," alisema Mrope.
Kwa upande wake dada yake Lwiza alisema kuwa yeye alipata taarifa kupitia kwa wanafunzi hao ambao alikuwa nao wakati wanatoka shule na kukimbizwa na watuhumiwa hao, ambapo walisema kuwa ilibidi warudi na kumkuta mwenzao akitokwa damu, wamkokota mwenzao hadi nyumba iliyojirani na kumjulisha.
"Alikuwa kwenye hali mbaya kwani alikuwa akitokwa na damu nyingi na nilipomuuliza alisema kuwa amebakwa na mtuhumiwa ambaye alimtambua na kumtaja jina mwenye umri wa miaka 10 akiwa na wenzake watatu," alisema Lwiza.
Lwiza alisema kuwa baada ya kuona hali ile walimpeleka shule na uongozi wa shule ukamwelekeza kufuata taratibu za kisheria ambapo walikwenda Serikali ya mtaa kisha kwenda polisi na baadaye Hospitali ya Tumbi kwa matibabu zaidi ambapo hadi juzi mwanafunzi huyo alikuwa bado kalazwa na hali yake inasemekana kuwa ni mbaya.
Naye Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Lulanzi, Anna Bilali alisema kuwa wao kama uongozi wa shule hawawezi kusema lolote kwani suala hilo liko kwenye vyombo vya sheria pamoja na kitabibu na watakuwa tayari kusema mara taarifa zitakapokamilika.
"Ni kweli tukio hili limetokea lakini bado haijathibitishwa kama ni kweli au la na pia lilitokea nje ya shule na muda wa shule kwa wanafunzi wa madarasa ya chini walisharuhusiwa kurudi nyumbani mara baada ya masomo kwisha," alisema Bilali.
Akizungumzia tukio hilo mjumbe wa mtaa wa Lulanzi, Rasul Shaban alisema kuwa walipata taarifa hiyo na kushangazwa na kitendo hicho ambapo tukio hilo ni la mara ya kwanza kutokea katika shule hiyo ambayo iko kwenye mtaa huo na pia walitoa barua za kuwadhamini wanafunzi wanaotuhumiwa kufanya tukio hilo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Ulrich Matei alisema kuwa hadi sasa wanawashikilia wanafunzi wanne wenye umri kati ya miaka 10 na 13 kuhusiana na tukio hilo
0 comments:
Chapisha Maoni