
Kumesambazwa picha ya noti ya shilingi mia tano yenye picha ya Mhe. Lowassa. Kitendo hicho siyo utani, bali ni dhihaka na dharau kwa alama za Utaifa na Mamlaka ya nchi. Lowassa Amesema hajui na wala ahusiki na usambazaji wa Noti hiyo Mitandaoni
Mhe. Lowassa anaheshimu maoni ya watu na nguvu ya mitandao ya kijamii, lakini anasisitiza umuhimu kwa wananchi kutumia nguvu hiyo ya mitandao kwa kujadili maendeleo ya nchi yetu badala ya kuwa watu wa kuzusha mambo yasiyo na tija kwa nchi yetu.
Imetolewa na:
Ofisi ya Mhe. Lowassa (MB)
0 comments:
Chapisha Maoni