00:49
0
Uchunguzi  wa kina unaonyesha kwamba wanawake  wengi waliojaaliwa  na mwenyezi Mungu Uzuri saana wa maumbo yao na sura zao hawaolewi,
Uchunguzi huo uliofanywa na mwandishi wetu unaonyesha wanawake watu wazima, au wasichana wanaochipukia ikiwa wamejaaliwa uzuri ule wa asili,na sio ule wa kununua, kama weupe wao,au maumbo yao yaliyojaa vizuri kila idara ya viungo vya miili yao,
Ngumu sana kuona wameolewa, uchunguzi huo ulioambatana na maswali kadhaa kutoka kwa akina dada wenyewe na baadhi ya wanaume umejaribu kumfanya mwandishi wetu kujiuliza maswali mengi  bila kupata majibu sahihi. 


Mwandishi wetu ametimba mpaka maeneo ambayo wanaume wengi  hujiuliza maswali wanapowaona wadada hao katika mishe mishe zao za style ya kutafuta maisha.
1. Sehemu za starehe yaani  clubs
2. Baa kubwa kubwa nchini.
3. Maeneo wanayopatikana madada poa
Madada wa kwenye baa  wengi majibu yao yalikua kama ifuatavyo.
Mwandishi:
Dada wewe mzuri sana, unaefaa kuwa mke wa mtu, unafikiri

nikwa nini unafanya kazi hii ambayo haina heshima kwa wanaokuona wanakuona kama malaya ?
Mhudumu wa baa:
Aaa kaka wanaume wengi ni michosho tuu, ukitoka kidogo akirudi maswali meengi kama polisi, mi nilishaolewa na nikaona michosho ya kupelekana  puta nikaamua kuachana na mume wangu na kuangalia mambo yangu, si unaona hii pete kaka, ni ya ndoa kabisaa ya kanisani.


Na hayo ndio majibu ya karibuni wadada woote aliopata nafasi ya kuwauliza maswali sehemu zoote silizooanishwa hapo juu.
Na wengine wa madada hao ni wasanii maarufu hapa Tanzania wa Bongo movie na wa musiki wa kizazi kipya. ‘Bongo fleva’ na baadhi ya watoto wa vigogo serikalini,na wenye nafasi kubwa ya kifedha nchini.
Majibu ya wanaume wengi walijibu kama ifuatavyo:

“Wanawake wazuri sana ni ugonjwa wa moyo,” “Wanaringa kuolewa kutegemea uzuri wao,” “Mwanamke mzuri lazima uwe na hela, Ili wenye hela wasikuzidi maarifa kwa hela zao”


Mmoja wa wanaume hao walipiga saluti kwa wadada mungu alivyowapendelea maumbo na kusema:
“Aaaa brother mi naogopa hata kuwaanza, na wanawake wengi hawana mapenzi ya dhati kwa dunia ya sasa, wanachoangalia wasilahi yao binafsi na sio ya kifamilia.
Jamani wapenzi wa ukurasa huu wa mahusiano,Nisaidieni kuongeza majibu ya walionijibu
Majibu niliyopewa ni sahihi kwa ufahamu wako?
Unafikiri ni kwa nini warembo hao hawaolewi?
Kazi kwenu.

0 comments:

Chapisha Maoni

rightcolbanner