03:23
0
Wiki iliyopita jarida la Vogue lilitoa picha ya jarada la jarida hilo na kuwaonesha Kanye West na Kim Kardashian wakiwa wamepoz kama watu wanaosubiri kufunga ndoa muda mfupi ujao au wanatoka kwenye tukio la ndoa.
Lakini baada ya kuanza kutolewa kwa picha za ndani za jarida hilo ambazo zinaionesha familia nzima ya bwana Kanye West, picha moja ilizua utata mkubwa hasa kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi walihoji kama kweli Kanye ni mtu wa kawaida ama ni ‘vampire’.


Kitu kilichopelekea kuzuka kwa swali hilo, ni picha inayomuonesha Kanye West akitumia iPad kuwapiga picha Kim Kardashian na mtoto wao North West huku Kim Kardashian nae akijipiga picha (selfie), lakini nyuma ya Kim Kardashian na North inaonekana kuna ukuta wenye kioo.

Utata: Ingawa Kanye West anaonekana kutazamana na kioo kile, taswira yake haionekani kwenye kioo hicho na ndipo wengi walipohoji uhalisia wa kile wanachokiona kama kweli jamaa ni binadamu wa kawaida.


Shouldn’t….shouldn’t Kanye West be in the mirror? Alitweet Katherin Mirror na kuambatanisha na picha hiyo.

Mtu mwingine alionesha kushangazwa zaidi na kudai kuwa picha hiyo itafundishwa kama kozi kwenye masomo ya uandishi wa habari miaka 100 ijayo.

“This photo is going to be taught in every media studies course of the next 100 years.” Alitweet Mett Novak.

Source:YAHOO.COM VIA BONGO61

0 comments:

Chapisha Maoni

rightcolbanner