15:26
0
Mwigizaji mkuu wa filamu hiyo Russell Crowe ©The Christian Post
Filamu mpya iitwayo Noah ambayo inatarajiwa kuzinduliwa mwezi wa nne mwaka huu tayari imepigwa marufuku kuonyeshwa katika mataifa matatu ya kiislamu kwa madai kwamba inakwenda kinyume na dini za mataifa yao.

Nchi ambazo tayari taarifa zake zimethibitishwa na mwandaaji wa Paramount pictures ambao ndio waliosimamia filamu hiyo ni pamoja na Qatar, umoja wa falme za Kiarabu (UAE)pamoja na Bahrain. Pia mataifa mengine ambayo yanauwezekano wa kutangaza kutoonyeshwa kwa filamu hiyo nchini mwao kwa kisingizio cha dini ni pamoja na Misri, Jordan pamoja na Kuwait.

Filamu hiyo ambayo imeandaliwa kwa kiasi cha dola milioni 125 za Marekani ikiigizwa na mwigizaji maarufu duniani Russell Crowe na waigizaji wengine, ni filamu inayosimulia kisa cha Nuhu kama kilivyoandikwa kwenye Biblia takatifu ingawa tayari kuna msuguano kutoka kwa baadhi ya watu ambao wanaamini waigizaji hao wa Hollywood wamechakachua baadhi ya mambo katika filamu hiyo. 

0 comments:

Chapisha Maoni

rightcolbanner