04:51
0


KUSHOTO: Pamela McCarthy (juu) na Jason Williams. KULIA: Pamela akikatiza mitaa huku akiwa uchi (juu) na kemikali za bafuni (chini).
Mama aliyempiga mtoto wake wa kiume mwenye miaka mitatu na kudaiwa kutaka kumshambulia kwa 'kemikali za bafuni' amenaswa na picha za kamera akikimbia uchi mitaani muda mfupi baada ya kumgundua.
Pamela McCarthy mwenye miaka 35 alikamatwa kwa kushitukizwa baada ya kupambana na vikosi vya askari nje ya makazi yake huko Munnsville, mjini New York, Jumanne iliyopita. Alifariki baadaye hospitalini.
Picha hizo za kushitusha, zilizopigwa na jirani, zimemuonesha Pamela akikimbia kuelekea aliko mwanae ambaye alikuwa amemng'ang'ania baba yake kwa hofu.
Majirani waliita polisi majira ya saa 1:45 usiku wakielezea mwanamke alikuwa akimpiga na kumkaba mwanae wa kiume, kushambulia majirani na kumnyonga mbwa wake mmoja.
Rafiki wa kiume wa mwanamke huyo, Jason Williams amesema alimwona mama huyo akikimbia uchi nje ya nyumba yao na kwenda kumkaba mtoto wao, ambaye Pamela alikuwa akimpiga na kujaribu kumvua nguo.
Katika mafuriko ya mashambulio ya nguvu nchi nzima, watuhumiwa wa 'kemikali za bafuni' wamekuwa wakivua nguo zao, wakidai dawa sanisi zilizokatazwa zimesababisha kuwaunguza.
Vikosi vya askari vilifika eneo la tukio, majirani wengine walilazimika kuripoti baada ya kuzidisha matumizi ya nguvu.
Jirani mmoja alisema: "Alikuwa...akikimbia huku na kule kuzunguka mtaa na akamkamata mbwa wake mmoja na kugalagala naye ardhini huku miguu yake ikiwa imemzingira mbwa huyo. Alikuwa akimkaba mbwa."
Mwingine alisema: "Ni wazi alikuwa akifanya sababu ya kitu fulani. Nani aliyefanya hivyo?"
Wakati maofisa walipofika eneo la tukio, walimkuta Pamela alikuwa 'akipigana kwa nguvu' na kwa wakati huo alikuwa akisukumwa na nguvu ya dawa, polisi walisema.
Askari walisema mwanamke huyo aliwakoromea wakati wakimkabili na kudai alijaribu kumng'ata mmoja wa maofisa.
Pale askari Christopher Budlong alipojaribu kumkamata Pamela, aligoma. Katika kujaribu kumtuliza, askari huyo akatumia maji ya pilipili kumpulizia, lakini haikufua dafu.
Kisha hapo akasambaza dawa ya kunyong'onyesa viungo na ndipo akaweza kumfunga pingu. Baada ya kufikishwa kituo cha polisi, akapatwa na mshituko wa moyo, polisi wamesema. Alikimbizwa hospitali lakini baadaye akafariki.
Jason alisema Pamela alikuwa na historia ya matumizi mabaya ya dawa lakini alihuzunishwa na tabia yake hiyo.
"Nilimweleza mama yake, 'anahitaji msaada'," Jason ameeleza. "Kila mmoja anasema tuachane naye sababu nimemueleza kila aina ya stori. Nakosa cha kusema. Nampenda...nampenda hadi mauti...kisha nashuhudia hilo."
Mtoto wake wa miaka mitatu alipelekwa kwa gari la wagonjwa hadi Hospitali ya Chuo Kikuu cha Upstate huko Syracuse na akatibiwa majeraha madogo. Hivi sasa anaishi kwa mama wa Jason.
Uchunguzi wa mwili wa Pamela utafanyika Jumatano ijayo kujua sababu za kifo chake.
Hili ni tukio la karibuni kabisa kuhusisha kemikali za bafuni, dawa zilizopigwa marufuku zinazodaiwa kuwa chanzo kwenye mashambulio mengi ya kutisha ambayo yanaibuka.

0 comments:

Chapisha Maoni

rightcolbanner