11:36
0
Bila shaka huu ni wakati muafaka sana ambapo inafaa kuwa na mjadala wa wazi kati ya Dr. W.Slaa na Dr. Kitila mkumbo juu ya "Tanzania na siasa tunayoitaka"

Nasema hivi kwa sababu, Kwa takriban miezi miwili mfululizo, Dr.Kitila amekuwa akiandika makala zenye maudhui mazito ambayo hayawezi kupuuzwa.Katika makala zake zote, zimekuwa zikionesha maudhui ya ujumla kwamba siasa za upinzani tanzania kwa sasa zimegeuka na kuwa ni sawa sawa tu na zile za CCM au pengine hata kuwa na udhaifu zaidi hata ya zile za CCM.kwa ujumla Dr.Kitila yeye anadhani pengine hilo linaweza kuwa ndio sababu kuu ya watanzania kuamua kuichagua CCM tu(LICHA YA UDHAIFU WAKE), huku upinzani ukianguka.

Kwa mfano Kitila Katika moja ta makala zake anasema "Vyama vingi vilipoanza, CCM walipanick sana wakawa wanawatukana sana wapinzani. Wakawapa kila aina ya majina: mbwa, wanafiki, wasaliti, n.k., kisa wanatofautiana na wao kimsimamo. Lakini leo hii baada ya upinzani (soma CHADEMA) kukua na kujipatia wafuasi nao wanaanza kufanya mambo hayohayo ya kijinga waliyofanya CCM miaka ya tisini: kukebehi, kukejeli, kuwapaka matope na kuwaita wasaliti watu wanaotofautiana nao kimwazo na misimamo. Wapinzani wamejikuta wanauvaa uCCM bila wao kujua."

Bila shaka unahitajika mjadala kati ya hawa Madaktari wawili ambao wote wana shahada ya juu ya falsafa (Dr.Slaa Vs Dr.Kitila), ili kupitia mjadala huo mambo haya yote yakawekwa sawa kwa hoja na vielelezo vya wazi na watanzania wakapata picha kutoka kwa watu wenye weledi na uelewa wajuu.

Naamini kama mjadala huo utafanyika, basi kutokea hapo, wadau wataweza kujadili wakiwa na msingi mzuri na imara wa marejeo, Badala ya utaratibu huu wa kila mtu kuibuka na kutoa hoja yake kwa wakati wake.
Credits:Jamii forums 

0 comments:

Chapisha Maoni

rightcolbanner