08:14
0

Ugonjwa wa homa ya nguruwe umelipuka tena mkoani Mbeya na kuua zaidi ya nguruwe 900 katika wilaya za Mbeya na Rungwe.
 
Mganga Mkuu wa Mifugo Mkoani Mbeya, Solomon Nong’ona akizungumza nasi jana alisema, ugonjwa huo umerudi tena baada ya kuzuka kwa mara ya kwanza Januari mwaka huu na kutokomezwa.
 
Alisema kufuatia kuzuka tena kwa ugonjwa huo, serikali kupitia sekta ya mifugo imepeleka dawa mkoani humo ambazo zinasaidia kupunguza kasi ya kuenea.
 
Nong’ona  alisema kufuatia kuzuka kwa ugonjwa huo wananchi nao wanajitahidi kununua dawa hizo ili kuudhibiti na kuwakinga nguruwe wanaowafuga.
 
Alisema ugonjwa wa homa ya nguruwe  bado haijathibitika kuwa na madhara kwa binadamu, hivyo wananchi wanaruhusiwa kula nyama ya nguruwe lakini aliyechinjwa katika machinjio rasmi na kuthibitishwa na daktari wa mifugo.
 
“Nguruwe hawa wanaweza kuliwa lakini wananchi wawe waangalifu kula nyama hizo kwani kula myama ambaye amekufa mwenyewe ni hatari kwani huenda amekufa kwa ugonjwa mwingine,” alisema Nong’ona.
 
Alisema ugonjwa huo ulianza katika wilaya ya Mbeya na baadaye katika wilaya ya Rungwe

0 comments:

Chapisha Maoni

rightcolbanner