Na Sweetbert Lukonge
KIUNGO wa Simba, Henry Joseph, amezua balaa katika kikosi cha timu hiyo baada ya kuonyesha uwezo wa kumudu na kucheza kwa ufanisi mkubwa nafasi mbalimbali uwanjani.
KIUNGO wa Simba, Henry Joseph, amezua balaa katika kikosi cha timu hiyo baada ya kuonyesha uwezo wa kumudu na kucheza kwa ufanisi mkubwa nafasi mbalimbali uwanjani.
Hali hiyo imewaogopesha baadhi ya wachezaji wenzake na kuwafanya wahofie kupoteza nafasi zao katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo ambayo inafundishwa na Mcroatia, Zdravko Lagarusic.
Baadhi ya wachezaji waliokumbwa na hofu hiyo ni pamoja na wale wanaocheza nafasi za beki wa kulia na kushoto ambao ni Said Nasoro ‘Chollo’, Shamte Ally na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’.
Hivi karibuni katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City, Henry alicheza nafasi ya beki wa kushoto na kuonyesha kiwango cha juu, pia katika mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Kinesi jijini, Logarusic amekuwa akimpanga Henry kama beki wa pembeni.
Logarusic alipoulizwa alisema: “Lengo langu ni kutaka kila mchezaji kucheza nafasi nyingi uwanjani, Henry ameweza kuonyesha kiwango cha juu katika kila nafasi, nitaendelea kumtumia ninapoona panapwaya.”
0 comments:
Chapisha Maoni