WAKATI mchakato wa Bunge la Katiba ukianza leo mjini Dodoma, ishu hiyo imemtia kwenye tope Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba baada ya kukwaa skendo ya ‘kutoka’ na mwigizaji Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ walipotimba mkoani humo.
Kwa mujibu wa staa wa filamu ambaye aliachwa katika safari hiyo ya kwenda kuhamasisha sanaa itambuliwe kwenye mchakato wa katiba mpya, Mwakifwamba alimteua Batuli ili akajiachie naye Dodoma kwa sababu hakuwa na vigezo.
“Akina Monalisa (Yvone-Cherry Ngatikwa) walistahili kwa ukongwe wao kwenye fani, sasa Batuli aliingiaje? Akili za kuambiwa changanya na zako,” alisema msanii huyo.
Akizungumzia skendo hiyo, Mwakifwamba alidai kuwa ameshasingiziwa vitu vingi hivyo anajua nyuma yake kuna kundi linalomchafua kila kukicha lakini ukweli ni kwamba hakumteua Batuli kwa lengo hilo.
“Sasa kama nimemteua kwa sababu hiyo, je, akina Monalisa nao niliwateua kwa kigezo hicho?” alihoji Mwakifwamba huku akikiri kuwa ameshaisikia sana skendo hiyo.
Kwa upande wake Batuli alifunguka: “Si kweli bwana, wameshatuzushia mambo kibao. Mara kuna fedha tumekula, mara sijui nini…sasa naona wamekuja na hili la mapenzi. Wabongo tuache majungu.
Katika safari ya Dodoma, mbali na Monalisa, wawili hao waliambatana na wasanii wengine wa tasnia mbalimbali wakiwemo Dude, John Kitime, P-Funk Majani na Abdul Salvador ambapo ndani ya bunge hilo linalotarajiwa kutikisa, wanawakilishwa na Paul Mtendah.
Credits:Global Publishers
0 comments:
Chapisha Maoni