10:36
0


Leo asubuhi dada yangu binamu amekuja home na talaka mkononi, ameachana na mume wake. Dada yangu amezaa na jamaa watoto watatu wa kwanza yuko kidato cha nne na wa mwisho hata darasa la kwanza hajaanza.
Kwa kweli sijaamini, na nimelia sanaaaa. Yani huwezi amini kilichotokea kwa sababu dada yangu ndo kwanza amefiwa na baba yake wiki mbili zilizopita, yani hata arobaini bado. Na jana ndo ametoka msibani huko mkoa ile kufika tu anakutana na talaka. So shemeji kashindwa hata kuvumilia mwenzie apooze machungu ya kuondokewa na mzazi.
Yani nimeumia, naogopa hata kuwaza kuolewa. Naanza kuamini ule msemo unaosema "Mwanaume sio ndugu yako."

0 comments:

Chapisha Maoni

rightcolbanner